You are currently viewing Mbowe: Mradi JNHPP usiishie kuwasha taa, bali uwe fursa ya maendeleo
Screenshot

Mbowe: Mradi JNHPP usiishie kuwasha taa, bali uwe fursa ya maendeleo

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema mradi wa kuzalisha Julius Nyerere (JNHPP), usiishie kuwasha taa pekee, bali uwe fursa za maendeleo ya vijijini.

Mbowe ameeleza hayo leo Agosti 22, 2026, katika uzinduzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) linalozalisha megawati 2,115, tukio lililofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Hatutegemei uwe umeme wa kuwasha taa peke yake,tunautegemea umeme huu ukawashe viwanda, huduma bora za kijamii na ukasaidie maendeleo vijijini. Umeme huu ukaleta furaha na mshikamano wa Watanzania waliokuwa na malalamiko ya kukosekana kwa nishati ya uhakika,”

Mbowe amesema Taifa limefanya kazi kubwa, huku akiwapongeza viongozi wa Serikali waliotanguliwa kwa kubuni mradi huo ambao Rais Samia ameiendeleza ndoto za watangulizi wake na umekamilika.

“Amesimamia mradi mradi kwa nguvu kubwa kwa kutumia fedha zetu za ndani.Hili ni jambo la kupongezwa na Watanzania wote wanapaswa kupongezwa kwa sababu ni sifa kubwa kwa Taifa,” amesema Mbowe.