SERIKALI ya Morocco imekubali kununua treni za mwendo kasi kutoka kwa kampuni ya Ufaransa ya Alstom, ukiwa moja ya mikataba iliotiwa saini wakati wa ziara ya Rais Emmanuel Macron, kwenye Ufalme huo, hatua inayoashiria kushuka kwa taharuki za kidiplomasia za muda mrefu.
Paris na Rabat kwa miaka mingi wamekuwa na taharuki ya mahusino katika miaka mitatu iliyopita hasa kuhusiana na masuala ya uhamiaji pamoja na eneo linalozozaniwa na Sahara Magharibi, ambalo Morocco inashinikiza jumuia ya kimataifa kulitambua kama sehemu yake.
Wakati akichukua hatua makini ili kujiepusha kukasirisha Algeria ambaye ni hasimu wa Morocco, Macron alilazimika kuunga mkono Morocco kwenye suala la Sahara Magharibi hapo Julai, hatua iliyofungua njia ya maridhiano.
Macron anafanya ziara ya Morocco akiandamana na mawaziri pamoja na wafanyabiasha 40 mashuhuri kutoka Ufaransa.
Akionyesha heshima isiyo ya kawaida, Mfalme Mohamed wa 5, wakati akitembelea kijiti, alimlaki Macron akiwa na mke wake Brigitte kwenye uwanja wa ndege jana Jumatatu, kabla ya kuanza kwa hafla ya kutia saini mikataba kwenye kasri ya Mfalme.
Shirika la reli la Morocco la ONFC, limetia saini mkataba na kampuni ya Ufaransa ya Alstom wa kununua mabehewa 12 ya mwendo kasi.