Hatimaye aliyekuwa Kada machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amehamia Chama cha Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibu Kamati kuu ya CCM kulikata jina lake kati ya wagombea waliokuwa wanaomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kutetea nafasi yake ya ubunge.

Hata hivyo, leo picha zilizopo kwenye ukurasa rasmi wa ACT Wazalendo zinamuonesha Kiongozi wa ACT wazalendo, Dorothy Semu, akimsajili Luhaga Mpina katika mfumo wa chama hicho kiganjani na kuwa mwanachama rasmi wa ACT Wazalendo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya siasa vinadai kuwa Mpina ambaye pia amesajiliwa mbele ya Zitto Kabwe, anatarajiwa kupeperusha bendera ya urais wa chama hicho kumvaa mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan.
