Mtoto Mwenye umri wa miaka nane Mkazi wa Uruira katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi amefariki dunia kwa kujinyonga huku chanzo kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo baada ya kutonunuliwa nguo za sikukuu za krimasi na mwaka mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema mzazi wa mtoto huyo, Matrida Kalidi aligundua mtoto wake, Christina Frank amejinyonga kwa kutumia sweta lake ndani ya chumba anacholala.
Aidha, Kamanda ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatimiza malezi bora kwa watoto wao ikiwemo kuwapatia mahitaji muhimu kama vile malazi na elimu.