You are currently viewing Muuguzi Arusha asimamishwa kazi madai ya kumbadilishia mzazi mtoto

Muuguzi Arusha asimamishwa kazi madai ya kumbadilishia mzazi mtoto

Wizara ya Afya imetangaza kumsimamisha kazi muuguzi aliyemhudumia mkazi wa Daraja mbili mkoani Arusha Bi. Neema Kilugala ambaye amedai kubadilishiwa mtoto.

Bi. Kilugala alijifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, Mount Meru tarehe 24 Machi, 2025

Katika taarifa iliyotolewa leo Aprili 2, 2025 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya, Roida Andusamile imesema wizara imechukua hatua hiuo ili kupisha uchunguzi. 

Pia imesema sampuli za wazazi waliojifungua kipindi hicho pamoja na za watoto zinachukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. 

Imesema kufuatia hali hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha pamoja na Jeshi la Polisi inatekeleza hatua hizo.

“Baada ya uchunguzi kukamilika taarifa rasmi zitatolewa na hatua stahiki zitachukuliwa,” imesema.

Katika ufafanuzi kuhusu taarifa hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijami, Bi. Neema anadai kuwa baada ya kujifungua alioneshwa mtoto wake na muuguzi akiwa ni mzima. 

Hata hivyo, aligundua kuwa amebadilishiwa mtoto wake baada ya kuletewa mtoto akiwa amefungwa na vitenge ambavyo si vya kwake.

Muuguzi wa hosptali hiyo alidai kuwa alichanganya vitenge na vya mtoto mwingine hivyo akaahidi kwenda kubadilisha, pamoja na kuchukua hatua hiyo bado kulikuwa na hali ya sintofahamu. 

Leave a Reply