You are currently viewing MwanaFa: Viwanja vyote vipo tayari kwa CHAN 

MwanaFa: Viwanja vyote vipo tayari kwa CHAN 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘ Mwana Fa’ amesema kuwa maandalizi ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani  (CHAN) yanaendelea kwa kasi, huku viwanja vyote vilivyopangwa kwa ajili ya mashindano hayo vikiwa tayari kwa matumizi hata kama michuano ingeanza mwezi ujao.

Kauli hiyo ametoa leo Mei 30, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, aliyeomba kuhakikishiwa kama Tanzania ipo tayari kwa CHAN inayotarajiwa kufanyika Agosti 2025.

Viwanja hivyo ambavyo Mhe Mwinjuma amesema vimekamilika ukarabati wake ni Benjamin Mkapa Dar es salaam, Amaan Zanzibar na viwanja vya mazoezi ambapo Dar es salaam kuna viwanja vitatu kikiwemo kiwanja cha Shule ya Sheria, Gymkana na Meja Jenerali  Isamuhyo ambavyo vyote vipo katika hali nzuri.

Leave a Reply