You are currently viewing Mwendesha mashtaka wa ICC achunguzwa kwa unyanyasaji kingono
Karim Khan

Mwendesha mashtaka wa ICC achunguzwa kwa unyanyasaji kingono

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu, ICC ya mjini The Hague, Päivi Kaukoranta amesema wameanzisha uchunguzi dhidi ya Mwendesha mashtaka mkuu Karim Khan anayetuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono.

Kaukoranta amesema jana Jumatatu kwamba chombo huru kitachunguza madai hayo ili kuhakikisha mchakato huo unakuwa huru, usioegamia upande wowote na wa haki.

Madai hayo yaliibuliwa mwezi Oktoba, lakini muhanga, ambaye ni mtumishi kwenye ofisi ya Khan aliripotiwa kuupinga uchunguzi na hakutaka kuyazungumzia madai hayo, hivyo kufanya uchunguzi huo kusitishwa.

Khan mwenyewe ameyapuuza madai hayo akisema hayana msingi na kuzihakikishia mamlaka kwamba yuko tayari kushirikiana na wachunguzi.

Leave a Reply