You are currently viewing Ndege iliyopotea yapatikana, abiria 50 wahofiwa kufariki dunia

Ndege iliyopotea yapatikana, abiria 50 wahofiwa kufariki dunia

Ndege ya abiria ya nchini Urusi iliyokuwa na watu takriban 50 imeanguka eneo la Amur, mashariki mwa nchi hiyo, huku watu wote waliokuwa ndani wakidhaniwa kupoteza maisha.

Ndege hiyo aina ya AN-24, inayomilikiwa na shirika la ndege la Angara, ilipotea kwenye rada ilipokuwa ikikaribia kutua katika mji wa Tynda, mkoani Amur, karibu na mpaka wa China.

Tukio la kupotea kwa Ndege hiyo, liliripotiwa kutokea asubuhi ya leo Julai 24, 2025, ambapo Gavana wa Mkoa wa Amur, Vasily Orlov alisema ilikuwa ikikaribia kutua katika mji wa Tynda, mkoani Amur, kabla ya kupoteza mawasiliano.

“Kulikuwa na abiria 43, wakiwemo watoto watano na wafanyakazi wa ndege sita,” alisema Gavana Orlov.

Mkoa wa Amur upo Mashariki ya Mbali mwa Russia, ukipakana na China upande wa kusini, kupitia Mto Amur l, ambao pia unatumika kama mpaka wa Kimataifa kati ya nchi hizo mbili.

Leave a Reply