You are currently viewing Ndege mpya ya Boeing iliyokwama jana kutua Zanzibar leo

Ndege mpya ya Boeing iliyokwama jana kutua Zanzibar leo

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Ndege mpya ya Boeing B8787- Dreamliner iliyokwama kuwasili jana Jumatatu Agosti 19, 2024 kutokana na changamoto ya hali ya hewa sasa kupokewa leo Jumanne Zanzibar.

Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa leo Jumanne Agosti 20, ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 inatarajiwa kutua saa 10:00 jioni kisiwani humo na kupokewa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanzibar.

Taarifa ilitolewa jana na kitengo cha uhusiano na mawasiliano kwa vyombo vya habari, Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inasema mabadiliko hayo yamesababishwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo ipo nje ya uwezo wao.

Leave a Reply