Kupitia Programu ya Uwekezaji kwa Jamii, Benki ya NMB imekabidhi misaada ya madawati 100, viti 100 na meza 100 kwa shule mbili za msingi na moja ya sekondari wilayani Malinyi, mkoani Morogoro, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 21.6.
Msaada huo ni sehemu ya Sh. Bil. 7.4 zilizotengwa na benki hiyo kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii katika Sektra za Elimu, Afya na Mazingira kwa mwaka 2026, ikiwa ni asilimia moja ya Faida Baada ya Kodi ya Mwaka wa Fedha ulioishia Desemba 31, 2025
.

Meneja wa NMB, Kanda ya Kati, Bi. Janeth Shango, ndiyealiyekabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe. Sebastian Waryuba, aliyeipokea kwa niaba ya walimu wakuu wa Shule za Msingi Madibila Chini, Salamiti na Shule ya SekondariKilosa Mpepo, zote za Malinyi.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika shule ya sekondari KilosaMpepo, Bi. Shango alisema Shule ya Madibila Chini imepewamadawati 50, idadi sawa na waliyopewa Shule ya Msingi Salamiti, huku Shule ya Sekondari ya Kilosa Mpepo ikisaidiwa viti 100 na meza 100 kwa ajili ya wanafunzi.
Msaada huu ni uthibitisho wa ushiriki wa Benki ya NMB katika maendeleo ya kijamii na kurejesha kwa jamii kutokana na faidawalioipata. Na ni kupitia michango hii, Benki ya NMB imewezakusaidia katika mbadiliko kwenye sekta ya elimu na pia kuifanyakutwa tuzo ya Benki Kinara wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Jarida la Global Banking and Magazine la Marekani.
Kwa upande wake, DC Waryuba, aliishukuru na Kuipongeza Benki ya NMB kwa msaada huu wenye thamani ya Sh. Mil. 21.6. hukuakibainisha kuwa kwa hesabu za haraka haraka utagundua kuwa kupitia madawati, viti na meza hizi, zinaenda kuwatoa sakafuniwatoto takribani 500 wa shule hizi waliokuwa wakisoma chini.
DC Waryuba aliongeza kuwa tayari NMB imefungua njia katika kuboresha elimu wilayani Malinyi na kuwataka wadau zaidi kufuatanyayo za benki hiyo kwa kujitolea kusaidia, huku akiwasisitizawalimu na wanafunzi umuhimu wa kutunza misaada hiyo ilikuwatia moyo wafadhili hao.
