Nyangumi mwenye nundu amefanya uhamiaji mkubwa na wa kipekee kuwahi kurekodiwa huku wanasayansi wakisema huenda uhamaji huo umechochewa na mabadiliko ya tabia nchi.
Dk. Ekaterina Kalashnikova kutoka kwa programu ya mamalia wa baharini Tanzania alisema kwamba tukio hili ni ”la kushangaza na la kipekee hata kwa aina hii ya wanyama wanaohama sana”.
Dk. Kalashnikova amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba umbali huu ni mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa kwa nyangumi aliye na nundu.
Amesema Nyangumi mwenye nundu huishi katika bahari zote ulimwenguni.
“Husafiri umbali mrefu kila mwaka na wana uhamiaji mrefu zaidi ya mamalia yoyote, wakisafiri kutoka maeneo ya uzalishaji ya kitropiki hadi maeneo ya chakula katika maji baridi.
“Lakini safari ya nyangumi huyu dume ilikuwa ya kipekee Zaidi, ikiwa na maeneo mawili mbalimbali ya uzalishaji.
“Nadharia moja ni kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanabadilisha wingi wa Krill – aina ya samaki ambao hutumika na nyangumi kama chakula chao hivyo basi kuwalazimu kuhamia bahari tofauti kutafuta chakula hicho.
”Ingawa sababu halisi bado hazijabainika ,lakini uhamiaji wa nyangumi wenye nundu huenda unachochewa na mabadiliko ya tabia nchi , mazingira mabaya ambayo yanatokea kila wakati na mabadiliko ya ya spishi,” amesema Dk. Kalashnikova.
Dume huyu aliyehama alikuwemo katika kundi la nyangumi wenye nundu ambao walinaswa katika picha kutoka kwa meli ya utafiti kwenye pwani ya pasifiki ya Colombia mwaka 2013.
Alitambuliwa tena katika eneo hilo hilo mwaka 2017 – na kando ya Zanzibar mwaka 2022.
Maeneo haya yanatenganishwa na umbali wa kilomita 13,046, ikiwa ndio umbali mfupi zaidi ambao nyangumi huyo angeweza kuchukua, wanasayansi wanasema ,ingawa inawezekana umbali huu ni mrefu zaidi.
Kwa kuwa dunia ni mduara, njia fupi zaidi kati ya maeneo mawili inatolewa kwa umbali wa mzunguko mkubwa, ambao ni sehemu inayounganisha sehemu mbili kwenye mduara.