Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema serikali imeanza mazungumzo yenye dhamira ya kuboresha maslahi ikiwemo makazi na posho kwa askari wote nchini ili kuweza kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kuwaongezea ujuzi na utaalamu ili kuendana na mazingira ya sasa ya kiuhalifu ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.
Ametoa rai hiyo leo Jumanne, wakati akizungumza na Maofisa, Wakaguzi, Askari wa Renk na Faili wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar pamoja na mikoa mitatu ya Unguja
