You are currently viewing Rais Dkt Samia alivyotimiza azma ya Kardinali Pengo

Rais Dkt Samia alivyotimiza azma ya Kardinali Pengo

Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi ameeleza namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan alivyoridhia kutoa ndege ya huduma za dharura kwa wagonjwa ili kufanikisha safari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kurejea nchini.

Dkt Nchimbi amefichua siri hiyo leo, Jumamosi Februari 28,2026 wakati akitoa salamu katika mazishi Kardinali Pengo yatakayofanyika Kituo cha Hija kilichopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa kuanzia Februari 12-15, Rais Dkt Samia alisafiri kikazi nchini Ethiopia na kwa utaratibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka ya urais alikabidhiwa yeye.

“Akiwa angani (Dkt Samia) ndipo nilipoletewa taarifa kuhusu hali ya Kardinali Pengo imebadilika, lakini alisisitiza kuwa chochote kitakachoweza kutokea kwake atafarijika kikitokea akiwa ndani ya ardhi ya Tanzania,” ameleeza Dkt Nchimbi.

Dkt Nchimbi anasema alipoombwa kusaidia ufanikishaji baada ya kuelezwa changamoto ya usafiri, alidhani ni jambo dogo kwa kuwa alikabidhiwa mamlaka na Rais Samia.

“Niliwasiliana na wenzangu akiwamo Waziri Mkuu, baadaye nilijua ni habari ya kubadilisha tiketi tu haraka haraka, ilipokuja taarifa kuwa kwa hali yake namna ya kumrudisha nyumbani (Pengo) kwa muda anaotaka yeye kuwahi lazima kukodi ndege ya ‘ambulance’,”

“Sasa hapo kwenye ndege ya ambulance hayo madaraka ya kurithi yalitaka kunitokea puani, washauri wakanielez kwa hatua hiyo lazima Rais afanye uamuzi.Nikamwandikia Rais ujumbe mrefu, akanijibu ameridhia ufanyike mchakato haraka sana,”

Balozi Nchimbi amesema pamoja na heshima kubwa ambayo Rais Dkt Samia ameitoa kwa Kardinali Pengo kwa kutambua mchango wake kwa Tanzania, lakini inatoa hamasa kwa Watanzania wengine wasio viongozi wa siasa kuonesha mapenzi kwa Taifa lao.

Leave a Reply