Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameondoka nchini leo Novemba 10, 2026, kuelekea jijini Antalya, Uturuki, kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Rais Samia ameagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, kabla ya kuanza safari hiyo.

Mkutano huo wa COP31 unawakutanisha viongozi na wadau mbalimbali kutoka mataifa tofauti kujadili masuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi na hatua za kukabiliana na athari zake.
Akiwa nchini humo, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (Antalya Leaders’ Summit), pamoja na kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika (High-Level Event on Clean Cooking in Africa).
