Rais Samia Suluhu Hassan, amepiga kura leo, Novemba 4, 2026, katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, katika Kituo Namba Tano kilichopo Ofisi ya Kijiji cha Chamwino.
Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Deogratius John Ndejembi, aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele, amesema Jimbo la Chamwino lina wagombea 16 wa nafasi ya ubunge, wakiwemo wanaume wanane na wanawake wanane, kila kundi likiwa na asilimia 50.
Aidha, wapiga kura 133,864 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo.
