You are currently viewing Rais Samia atuma ujumbe maalumu kwa Katibu Mkuu UN

Rais Samia atuma ujumbe maalumu kwa Katibu Mkuu UN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo  amewasilisha ujumbe maalumu wa Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ( UN), António Guterres  na kusisitiza dhamira ya nchi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu.

Baada ya mazungumzo yao, Balozi Kombo alimkabidhi Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  na Rais wa Kwanza wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa katibu Mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.