Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake, Rais wa Angola, João Lourenço, wamezindua Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere iliyopo Kilamba jijini Luanda.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Agosti 1, 2026 ukishuhudiwa na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere na viongozi mbalimbali.

Hospitali hiyo imepewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ikiwa ni heshima kwa mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, hususan nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Angola.
Hatua hiyo inaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Angola, uliyojengwa wakati wa harakati za kupigania uhuru na ukombozi wa mataifa ya Kusini mwa Afrika.
