You are currently viewing Rais Samia: Mchakato Katiba Mpya kuanza ndani ya siku 100

Rais Samia: Mchakato Katiba Mpya kuanza ndani ya siku 100

Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 100 pindi Watanzania watakapompa ridhaa Oktoba 2025.

Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo wakati akifungua kampeni za chama hicho, zilizohudhuriwa na umati wa wananchi katika Uwanja wa Tanganyika Packers Kawe, jijini Dar es Salaam.

Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ulikwama tangu mwaka 2014, kwa sababu mbalimbali, lakini tangu Rais Dkt Samia ashike madaraka mwaka 2021, ameonyesha dhamira ya dhati ya kuurejesha kwa kuanza kuunda kikosi kazi kilichokusanya na kuchakata maoni ya wadau wa demokrasia.

Kwa ahadi ya Dkt Samia leo Alhamisi mbele ya maelfu ya Watanzania ni dhahiri mkuu huyo wa nchi, anakwenda kuukwamua mchakato huo ambao kwa nyakati tofauti wadau wa demokrasia wamekuwa wakishauri ufanyiwe kazi.

“Katika siku 100, kupitia falsafa ya 4R ataendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda tume ya kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya,” amesema na kuongeza kuwa

“Tutaendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda tume ya kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya,” amesema Dkt Samia katika mkutano huo.

Leave a Reply