Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mustakabali wa Afrika unategemea afya na ustawi wa wananchi wake, akisisitiza umuhimu wa nchi za bara hilo kuwekeza katika huduma za afya ya mama, mtoto na vijana ili kujenga jamii yenye afya na kuchochea maendeleo endelevu.
Amesema kuhakikisha wajawazito wanapata huduma bora za afya, kulinda watoto na kuwekeza kwa vijana ni hatua muhimu katika kujenga kizazi chenye afya, uwezo na nguvu ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya bara la Afrika.
Dkt. Samia ameyasema hayo Novemba 23, 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa uzinduzi wa Mpango Elekezi wa Umoja wa Afrika wa Mabingwa wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto na Vijana wa mwaka 2026–2030, uliofanyika sambamba na ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026).
Akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya afya, Dkt. Samia amesema: “Kwa hakika, mustakabali wa Afrika unategemea afya na ustawi wa wananchi wake. Kulinda afya za akina mama, watoto na kuwekeza kwa vijana ni wajibu wa msingi wa viongozi.”
#SamiaKinaraAfrika
#AfyaMamaNaMtoto
