You are currently viewing Rais Samia: Sasa ni wakati wa maridhiano

Rais Samia: Sasa ni wakati wa maridhiano

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mazugumzo na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, huku akisema ni wakati mwingine wa kuendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Novemba 16, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa kikao hicho kimefanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Rais Samia amelishukuru Baraza hilo pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kwa utayari wao wa siku zote za kufanya mazungumzo ya majadiliano yha kuimarisha misingi ya Taifa letu.

“Sasa ni wakati mwingine wa kuendeleza mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi kwa kuunda Tume ya Maridhiano na upatanishi, itakayoratibu maandalizi ya mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania,” imeeleza.

Kikao cha Rais Samia na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kinaendeleza hatua za mashauriano ya Mkuu huyo wa nchi na wadau mbalimbali kuhusu mchakato huo wa maridhiano.