Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka vijana Watanzania kuilinda amani ya Taifa kwa kulindana wenyewe na kuonesha dunia kuwa yaliyokea Oktoba 29, 2025 hayatatokea tena.
Amesema yaliyotokea Oktoba 29,2025 yalilitia doa Taifa hasa kwa kuwa inaaminika Tanzania ni nchi ya amani hivyo vijana wanamchango mkubwa wa kurejesha amani hiyo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Mei 8,2026 wakati akizungumza na wananchi makundi ya mama lishe, machinga na vijana waliovaa fulana zenye maandishi ya ‘Never Again’ waliojitokeza kumsalimia, wakati akianza safari yake ya kutokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kwa shughuli za kikazi.
“Vijana wangu nimepokea ujumbe wenu, na niwaombe sana kama kweli mmekusudia ‘Never Again’ kama fulana zenu zinavyosema, naomba mlindane wenyewe kwa wenyewe na msikubali kutiwa maneno ya kuharibu usalama wa nchi yetu na nchi yetu kwa ujumla,” amesema Rais Samia.
