You are currently viewing Rais wa Angola atembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi Afrika

Rais wa Angola atembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi Afrika

Rais wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, akipokea Kamusi ya Kiswahili kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, alipotembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 29, 2026.

Rais João Lourenço yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu, kuanzia Oktoba 28 hadi 30, 2026, kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais huyo awali amepokelewa na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, Oktoba 29, 2026.

Baada ya kuwasili Ikulu, Rais Lourenço amekagua gwaride rasmi la mapokezi lililoandaliwa kwa heshima yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Baada ya mapokezi hayo, Rais Samia ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na ujumbe wa Angola ulioongozwa na Rais Lourenço.