You are currently viewing Rwanda yakana Kagame kuwa mahututi
Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Rwanda yakana Kagame kuwa mahututi

Jeshi la Rwanda limesema kuwa madai ya kwamba afya ya Rais Paul Kagame iko hatarini sana ni habari za hongo.

Kauli hiyo imekuja kutokana na taarifa mbalimbali kuibuka kuhusu afya ya Rais Kagame baada ya kutoonekana hadharani kwa takribani wiki tatu.

David Himbara, kiongozi wa upinzani anayeishi uhamishoni na mshauri wa zamani wa masuala ya kiuchumi wa Kagame hivi karibuni amekuwa akidai kuwa Rais Kagame ni mgonjwa na kwamba yuko Ujerumani.

Gazeti la Rwanda la Taarifa lilimnukuu msemaji wa serikali Yolande Makolo akisema kuwa Rais Kagame ni binadamu kama kila mtu ambaye huchukua muda kupumzika.

Gazeti hilo linamnukuu Makolo akisema: “Rais yuko vizuri na anapumzika kawaida.” Kutoonekana kwa Rais Kagame hivi majuzi kumetolewa maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii na katika mazungumzo ya faragha.

Rais Kagame alionekana hadharani kwa mara ya mwisho tarehe 6 mwezi huu alipokaribisha kikundi kutoka Shule ya Hope Haven Christian School mjini Kigali, Rwanda.

Leave a Reply