You are currently viewing Samia alivyojipanga kujenga, kuboresha barabara Kilimanjaro

Samia alivyojipanga kujenga, kuboresha barabara Kilimanjaro

Baada ya hatua kubwa zilizopigwa katika sekta za afya, umeme, afya na elimu mkoani Kilimanjaro, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuhamishia nguvu katika uboreshaji na ujenzi barabara za mkoa huo.

Katika maelezo yake, Dkt Samia amesema sekta za maji, elimu, umeme na afya Serikali imefanya kazi nzuri, akitolea mfano hivi sasa mkazi wa Kilimanjaro halazimiki kwenda Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI),Dar es Salaam kufuata huduma kwa sababu zinapatikana mkoani humo.

“Kipaumbele chenu wananchi wa Kilimanjaro na kote nilikopita ni miundombinu ya barabara. Hapa Moshi Mjini tutajenga barabara ya mchepuko ya Kae hadi uwanja ndege yenye urefu wa kilomita 31,” amesema Dkt Samia.

Dkt Samia ametoa ahadi hiyo, leo Oktoba Mosi,2025 akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa,Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika mwendelezo wa kampeni za kusaka kura mkoani hapa.

Pia, Dkt Samia amesema fedha zimeshatengwa za ujenzi wa barabara ya kilomita 10 kupitia mradi wa uendelezaji wa miji utakaotekelezwa mji wa Moshi.

Kwa Moshi Vijijini, Dkt Samia ameahidi kukamilisha barabara za Moshi International School-Kibosho Kati kwa Rafael yenye urefu wa kilomita 13.

“Lakini pia barabara ya Kidia-Urisini yenye kilomita 10, barabara ya Mamboleo- Shimbwe kilomita 10.3, barabara ya Rau-Madukani-Mamboleo- Materuni kilomita 10, barabara ya Samanga-Chemchem kilomita 10,”

“Barabara zote zinajengwa na zimefikia katika hatua mbalimbali, tunakwenda kuzikamilisha kwa kiwango cha lami,” ameeleza Dkt Samia.

Ameendeleza kueleza kuwa kwa upande wa Jimbo la Vunjo, Dkt Samia ameahidi kukamilisha barabara za Pofu- Mandaka- Kilema yenye urefu kilomita 10 ambayo ni tegemeo la wananchi na watalii wanaoshuka Mlima wa Kilimanjaro.

Katika jimbo hilo hilo, Dkt Samia ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara ya kipekee, Uchira- Kisomachi ambayo wananchi walianza mchakato huo kwa nguvu zao, kisha Serikali ikaongeza nguvu.

Dkt Samia hakuiacha Same, alikoeleza kuna kuna tatizo hasa milimani ambako nyakati za mvua maji yanashuka chini, akiahidi timu ya watalaamu kufanya utafiti kisha ujenzi wa barabara wa kiwango cha lami ngumu utafuata.

“Kule Rombo tutakamilisha ujenzi wa barabara ya kimkakati ya kukuza biashara mpakani kati ya jirani zetu Kenya kupitia barabara ya Horiri- Tarakea yenye kilomita 53,” amesema Dkt Samia.

Kuhusu wananchi wa Moshi Vijijini wanaosifika kwa kulima kahawa, Dkt Samia amewaahidi kuwaanzisha vituo vya ukodishaji wa zana bora za kilimo ili kuwawezesha kufanya kilimo chao kwa gharama nafuu zaidi.

Katika hatua nyingine, Dkt Samia amesema ndani ya miaka mitajo ijayo atakwenda kukamilisha m

Leave a Reply