Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dodoma, leo Jumatatu tarehe 26, Mei 2025.
Katika kikao hicho pia amehudhuria Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wassira ambaye wiki kadhaa zilizopita alizua gumzo baada ya kutoonekana katika ziara za chama hicho hali iliyomlazimu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Amos Makalla kudai kuwa amepumzika.