Rais Samia Suluhu Hassan, ametaka shangwe zilizoshuhudiwa katika Tamasha la Kizimkazi 2026, zigeuzwe kuwa fursa ya maendeleo zitakazowagusa na kustawisha maendeleo ya wananchi.
Amesema shangwe mara nyingi ni nzuri na inawaleta wananchi pamoja, kuimarisha mshikamano, umoja na kutangaza utamaduni pamoja na kuvutia wageni.
Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo Agosti 14, 2026 wakati wa Kilele cha Tamasha la Kizimkazi, katika Viwanja vya Mwehe, Kusini Unguja.
“Shangwe iwe lango la fursa na fursa hizo ziwe chanzo cha ustawi wa wananchi wetu na Taifa kwa ujumla. Baada ya shangwe hilo kumalizika, wananchi wabaki na huduma, miundombinu, biashara na fursa zinazoweza kufanya kazi,” amesema.
