You are currently viewing Samia ateua, apangua wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Samia ateua, apangua wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi serikalini kwa kuwahamisha na kuwateua viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya, wizara na taasisi za umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, mabadiliko hayo yanajumuisha:

  • Wakuu wa Mikoa wapya: Balozi Simon Sirro (Kigoma), Mboni Mhita (Shinyanga), Beno Malisa (Mbeya), Kheri James (Iringa), na Jabir Makame (Songwe).
  • Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa: Kenan Kihongosi ahamishiwa Arusha; Anamringi Macha ahamishiwa Simiyu.
  • Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu: Agnes Meena (Wizara ya Mifugo), Dk. Hussein Omar (Elimu), Prof. Makenga na Mhandisi Kilundumya (mazingira na kilimo).
  • Makatibu Tawala wa Mikoa wapya: Abdul Mhinte (Dar es Salaam), Dk. Frank Hawasi (Songwe), pamoja na uhamisho wa wengine wawili kati ya Pwani na Tanga.
  • Wakuu wa Wilaya wapya: 17 wameteuliwa, akiwemo Mikaya Dalmia (Kigamboni), Thecla Mkuchika (Butiama), Benjamin Sitta (Iringa), na wengine.
  • Wakurugenzi wa Halmashauri: 12 wapya wameteuliwa, huku wengine wawili wakihamishwa.
  • Uteuzi wa Mkuu wa Taasisi: Mhandisi Machibya Masanja kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Leave a Reply