You are currently viewing Samia: Hakutakuwa na tishio la usalama siku ya uchaguzi

Samia: Hakutakuwa na tishio la usalama siku ya uchaguzi

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuhusu usalama siku ya upigaji kura, akisema Serikali yake imejipanga vema.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumapili Septemba 28, 2025 alipozungumza na wananchi wa Msata mkoani Pwani, akiwa safarini kwenda mkoani Tanga kwa ziara ya kampeni za urais.

Ameeleza hakutakuwa na tishio lolote la kiusalama, kwa kuwa Serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha matishio yote yanadhibitiwa. 

“Nalotaka kuwahakikishia hakutakuwa na tishio lolote la kuisalama, tumejipanga vizuri mno, tumejipanga vizuri, hakuna tishio la kiusalama asitokee mtu kuwatisha.

“Yamewashinda wenyewe kuingia kwenye mashindano wasiharibu upigaji wa kura, kwa hiyo hakuna tishio tokeni kapigeni kura,” amesema.

Leave a Reply