You are currently viewing Samia: Huduma bora za afya ni haki kwa kila Mtanzania

Samia: Huduma bora za afya ni haki kwa kila Mtanzania

Rais Samia Suluh inu Hassan, amesema malengo ya Serikali ni kuhakikisha huduma bora za afya zinakuwa haki kwa kila Mtanzania.

Ili kutimiza hilo, amesema katika mwaka wa fedha 2026/27 Serikali imetanga Sh1.8 trilioni kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vya afya ikiwemo kuboresha huduma, dawa na vifaa tiba.

Rais Samia ameeleza hayo leo, Juni 24, 2026 wakati akizindua jengo la tiba ya mionzi kwa ajili ya wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Tunafanya hivi tukitambua uwekezaji katika afya, ni uwekezaji katika nguvu ya Taifa na ustawi wa familia zetu. Tunapoendelea na safari ya maendeleo, Taifa letu linaanza utekeleza wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo,” amesema.

Amesema malengo yaliyowekwa na Dira ya Taifa ya 2050 hayatatimia, iwapo hakutakuwa na watu wenye afya na uwezo wa kushiriki kikamiifu katika shughuli za kiuchumi, ndio maana tunatoa kipaumbele katika sekta ya afya.