You are currently viewing Samia kujenga Machinga Complex Iringa

Samia kujenga Machinga Complex Iringa

Kama ulidhani Machinga Complex ni stahiki ya Dar es Salaam pekee, jengo kama hilo litakuwepo pia katika Mkoa wa Iringa kama ilivyoahidiwa na Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan.

Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumapili Septemba 7, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais Iringa Mjini, mkoani Iringa.

“Tumeanza taratibu za kutafuta fedha kujenga Machinga Complex ndani ya Mji wa Iringa. Hili ni hamu yangu nimaliza kabla sijamaliza awamu hii ya uongozi,” amesema.

Amesema jengo hilo, analenga litumiwe na wafanyabiashara wadogo, wakiwemo mamalishe na wengine.

Sambamba na hilo, amesema katika uongozi wake amefanikisha upatikanaji wa fedha za ujenzi wa ofisi ya machinga mkoani humo.

Leave a Reply