SERIKALI kupitia Ofsi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajra na Wenye Ulemavu Ofisi imetangaza ufadhili wa ada ya mafunzo kwa asilimia 100 kwa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani mbalimbali zinazotolewa na vyuo vinavyotambuliwa na VETA.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo imeeataka vijana hap kufika katika vyuo vya VETA vya Mikoa na Wilaya pamoja na vyuo vilivyoainishwa na ofisi hiyo ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo.
“Mwanafunzi mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani,” imesema taarifa hiyo.
Imefafanua kuwa ufadhili huo unatokana na Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.
“Ofisi imeingia makubalano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi ambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbati zikljumuisha ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashl, Useremala, Uchomeleaji na uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi ya alama, Upishi, Utengenezajl wa vipuri vya mltambo, Ufundi Magari na Mitambo, umeme wa majumbani na vlwandanl, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utal, Ukataji Madini na Ufundi vyuma.”
Ili kupata orodha ya vyuo hivyo tazama hapa.https://www.kazi.go.tz/uploads/documents/en-1738402068-ORODHA%20YA%20VYUO%20VILIVYOKUBALIKA%20NA%20SERIKALI%20KUTOA%20MAFUNZO.pdf