You are currently viewing Simai: Tusiyumbishwe na siasa za urais 2030, tumheshimu Dkt Samia

Simai: Tusiyumbishwe na siasa za urais 2030, tumheshimu Dkt Samia

Na Mwandishi Wetu

Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said, amewaonya wanaofanya siasa za urais mapema, akisisitiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kumheshimu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuelekeza nguvu katika kuwatumikia wananchi badala ya kuanza makundi ya kisiasa.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Ijumaa Mei 22, 2026 Simai amesema baadhi ya watu wameanza harakati za chinichini kutafuta urais wa 2030, akisema hatua hiyo inaweza kuvuruga umoja ndani ya chama.

Amesisitiza kuwa wanachama wanapaswa kusimama pamoja nyuma ya Dkt Samia kama mwenyekiti wa chama na alama ya mshikamano wa taifa.

“Tusikubali kuchanganywa kuelekea 2030. Sasa ni muda wa kufanya kazi, kutekeleza ilani na kuhakikisha vijana wanapata ajira,” amesema Simai. ‎