You are currently viewing Tanzania, Kenya zasaini mikataba nane

Tanzania, Kenya zasaini mikataba nane

Serikali ya Tanzania na Kenya zimesaini mikataba nane ya ushirikiano, ikiwa ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa mataifa hayo.

Mikataba hiyo imetiwa saini leo, Jumatatu Mei 4, 2026 mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na William Ruto wa Kenya, aliyekuja nchini kwa ziara ya siku mbili.

Mikataba iliyosainiwa ni ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar kwenda Mombasa Kenya na mkataba wa kuuziana umeme njia moja imekamilika bado moja ambayo imesainiwa leo.

Katiba hotuba yake, Dkt Samia amesema mikataba mingine ni wa makubaliano kwenye sekta ya uchukuzi na miundombinu ambapo wamesaini ujenzi  wa reli kutoka tanga bandari kilimanjaro hadi Taveta Kenya.

“Kwenye hili pia Rais Ruto amesema kuna kipande kingine ambacho nacho tutaunga kwenye SGR kutoka Kenya hadi Singida,” amesema Rais Samia.

Eneo lingine kwenye uchukuzi ni Kuunganisha usafiri na usafirishaji wa maji hasa katika Ziwa Victoria ambalo linaunganisha nchi za Kenya na Uganda.

“Kwenye ulinzi ugaidi, dawa za kulevya, uhamiai haramu so tumekubaliana kuongeza nguvu ili watu waovu wasivuke upande wowote wa nchi zetu mbili,” amesema.

Sekta zingine ni Anga, Tehama na Kilimo; “ Sisi Tanzania tunalima sana tumeomba wafanya biashara waje kununua mahindi Tanzania na kwenda kuyauza na serikali hizi mbili pia ziuziane mazao,” amesema.