You are currently viewing Tanzania kuna utulivu, hakuna chokochoko za udini

Tanzania kuna utulivu, hakuna chokochoko za udini

Katibu  wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT),  Askofu Israel Maasa, amesema kwa zaidi ya nusu karne, Watanzania wa dini zote wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani na utulivu.

Mbali na hilo, amesema Watanzania wamekuwa wakiishi kwa kushirikiana katika maendeleo ya Taifa, kuoana baina ya familia za dini tofauti, kufanya biashara pamoja, kujenga urafiki na kuendeleza utamaduni wa kuheshimiana.

Askofu Maasa ameeleza hayo leo Jumanne Mei 26,2026 wakato akizungumza na wanahabari kwenye mkutano ulioandaliwa na JMAT uliofanyika jijini Dodoma.

Amefafanua kuwa hatua hiyo imeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yenyeutulivu mkubwa barani Afrika.

” Tuhuma na shutuma hizi dhidi ya uwepo wa ubaguzi wa kidini nchini Tanzania zimetusikitisha, kutukasirisha na kutufedhehesha.

“Raia wa Marekani wanaoishi Tanzania ni mashahidi wa kushamiri kwa uhuru wa kuabudu hapa nchini.Hatutaki kuamini kwamba Marekani Taifa ambalo sote tuliumizwa na kulia pamoja wakati wa mashambulizi ya kigaidi kwenye Ubalozi wake jijini Dar es Salaam mwaka 1998,”

” Kwa sababu hiyo, JMAT inalitaka Bunge la Marekani kukataa hoja hii ya kibaguzi ya maseneta wake kwani haina ukweli wowote na ina lengo la kupandikiza chuki ambazo hazipo nchini,”

Katika hatua nyingine, JMAT imeitaka Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ifanye mapitio ya uhusiano wa kidiplomasia na ya nchi baina ya Tanzania na Marekani, ili pamoja na mambo mengine, iweke msimamo wa kukataa na kutovumilia uchonganishi wa kidini unaoweza kuliingiza taifa letu kwenye matatizo makubwa.

Aidha, JMAT imesema Dkt Samia ameonyesha nia ya dhati ya kuchukua hatua dhidi ya mapungufu yaliyotokea mwaka 2025 ikiwa ni pamoja na kuunda Tume ya Uchunguzi na nyingine ya kijinai ili uwajibikaji wa haki na maridhiano vichukue nafasi na kuwezesha kupatikana kwa Katiba Mpya kama ambavyo ameahidi.