You are currently viewing Tanzania yaibuka kidedea ujumbe kamati ya urithi wa Dunia Unesco
Screenshot

Tanzania yaibuka kidedea ujumbe kamati ya urithi wa Dunia Unesco

Tanzania imeshinda kiti cha Ujumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya Unesco (World Heritage Committee) katika uchaguzi uliofanyika Novemba 24,2025 jijini Paris, Ufaransa.

Kamati ya Urithi wa Dunia ni chombo maalumu ndani ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ( Unesco). Tanzania itadumu katika ujumbe huo kwa miaka minne 2025/29

Chombo hicho kina jukumu la kusimamia na kulinda maeneo yaliyo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia.

Majukumu ya makuu ya kamati hiyo ni pamoja na kupokea na mapendekezo ya  maeneo mapya yanayopendekezwa na nchi wanachama kuingizwa katika orodha ya Urithi wa Dunia.

Pia,  kuamua maeneo gani yanakidhi vigezo vya ‘urithi wa kipekee wa kibinadamu (outstanding universal value’ ili kuorodheshwe rasmi.

Sambamba na hilo, kamati hiyo ina jukumu la kufuatilia hali ya uhifadhi wa maeneo yote yaliyoko kwenye orodha.

Leave a Reply