You are currently viewing Tanzania yajipanga kwa “Miss World 2027”

Tanzania yajipanga kwa “Miss World 2027”

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Tanzania kuanza maandalizi ya kuwa mwenyeji wa shindano urembo duniani (Miss World) mwaka 2027.

Uamuzi huo unatajwa kuwa utafungua mafanikio lukuki kwa nchini ikiwemo katika uendelezaji wa vipaji, sanaa na utalii na zaidi kukuza chapa (brand) ya nchi katika dunia hii iliyosheheni ushindani.

 

Hayo yamebainishwa leo Visiwani Zanzibar ambapo Rais Samia @samia_suluhu_hassan alipozialika sekta mbili za @wizara_sanaatz na @wizarayamaliasilinautalii kushiriki mazungumzo na Kamati ya Mashindando ya Unyange Duniani (Miss World).

Wanakamati waliofika nchini ni pamoja na Rais wa Kamati hiyo Mama Julia Morley (CBE), Mnyange wa Dunia wa sasa @suchaaata na Mnyage wa Afrika @hasset_dereje kujadiliana maendeleo ya sekta hiyo. 

“Ukiondoa matukio ya awali yanayokwenda mwaka mzima, fainali pekee ya Unyange Duniani ambayo huhudhuriwa na takribani watu 5,000 ukumbini, tukio hilo kubwa duniani husomwa, hutazamwa na kufuatiliwa na watu zaidi ya bilioni diniani,” amesema Dkt. Hassan Abbasi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili mara baada ya kikao hicho muhimu akifafanua namna utalii utakavyonufaika. 

Leave a Reply