Tanzania imetumia Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kuendeleza msukumo wake wa kutaka Kiswahili kitambulike na kuwa miongoni mwa lugha rasmi za kazi za umoja huo.
Hayo yameelezwa leo, Oktoba 6, 2026 na Mbunge na Mwakilishi wa Tanzania katika Mkutano wa 153 wa IPU, Dk Damas Ndumbaro, unaofanyika jijini Arusha na kukutanisha zaidi ya wajumbe 2000 kutoka mataifa 184 duniani.
Amesema Kiswahili ni lugha pekee ya asili ya Afrika yenye hadhi ya kimataifa inayozungumzwa na zaidi ya watu milioni 200, hivyo kinastahili nafasi kubwa zaidi katika taasisi za kimataifa.
“Ujumuishi huanza na lugha ya wananchi. Tanzania inarudia wito wake wa kutaka Kiswahili kitambuliwe kama lugha rasmi ya kazi ya IPU,” amesema.
