You are currently viewing Trump azuia mpango wa Israel kumuua kiongozi mkuu Iran

Trump azuia mpango wa Israel kumuua kiongozi mkuu Iran

Rais wa Marekani, Donald Trump amepinga mpango wa Israel wa kumuua kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Ofisa mkuu wa Marekani ameliambia shirika la habari la AFP kuwa “Tuligundua kwamba Waisraeli walikuwa na mipango ya kumpiga kiongozi mkuu wa Iran. Rais Trump alikuwa kinyume na hilo na tuliwaambia Waisraeli wasifanye hivyo.”

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema “Lakini naweza kukuambia zaidi… tutafanya kile tunachohitaji kufanya na nadhani Marekani inajua ni nini kizuri kwa Marekani,” alisema.

Kauli hiyo imekuja wakati Israel na Iran zikibadilishana safu nyingine ya makombora jana Jumapili, huku wakaazi wakiambiwa watafute makazi huku milipuko ikisikika juu huko Jerusalem, na mifumo ya ulinzi wa angani ikiripotiwa kuwashwa mjini Tehran.

Baada ya miongo kadhaa ya uadui na vita vya muda mrefu vilivyopiganwa kupitia washirika na operesheni za siri, mzozo wa hivi karibuni uliashiria mara ya kwanza kwa nchi hizo kubadilishana makombora kwa nguvu kama hiyo, na kusababisha hofu ya mzozo mrefu ambao unaweza kukumba Mashariki ya Kati nzima.

Ilianza siku ya Ijumaa, wakati Israel ilipoanzisha mashambulizi ambayo yaliwaua makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia, na kushambulia kambi za kijeshi, maeneo ya nyuklia na maeneo ya makazi kote nchini.

Shambulio la Tel Aviv bila sababu lilisababisha mzozo huo, na kuifanya Iran kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel.

Mashambulizi na majibu ya mashambulio yameendelea tangu wakati huo.

Leave a Reply