You are currently viewing Trump kuteta na marais 5 kutoka Afrika
Donald Trump

Trump kuteta na marais 5 kutoka Afrika

Rais wa Marekani Donald Trump juma lijalo atawakaribisha katika ikulu yake viongozi kutoka mataifa matano ya Afrika, ambapo watajadiliana kuhusu fursa za kibiashara.

 Marais kutoka nchi za Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal ndio watakaoshiriki mazungumzo na Rais Trump.

Mmoja wa mofisa wa White House amesema, Trump anaamini mataifa ya Afrika yanatoa fursa kubwa za kiuchumi ambazo hazifaidi tu Marekani pekee lakini bara Afrika.

Mkutano huo wa Juni 9 hadi 11 unajiri wakati huu utawala wa Trump ukiwa umekatisha ufadhili wake wa kigeni, msaada ambao mataifa mengi ya Afrika yalikuwa yakiutegemea.

Jumanne ya wiki hii, Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio alithibitisha kuwa nchi yake inaachana na misaada yake kwa mataifa ya kigeni na kwamba itajihusisha tu na nchi zinazoonyesha uwezo wa kujisadia kutatua changamoto zake.

Leave a Reply