You are currently viewing Ujenzi daraja la Jangwani waiva, Bashungwa ashuhudia utiaji saini

Ujenzi daraja la Jangwani waiva, Bashungwa ashuhudia utiaji saini

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 22 Oktoba 2024 ameshuhudia utiaji saini, ujenzi wa daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 litakalounganisha kipande cha Magomeni Wilaya ya Kinondoni na Jangwani Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ukumbi wa Karimjee-Posta na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya wa Ilala, wajumbe wa vyama vya siasa, Wakurugenzi,Madiwani, wabunge wasimamizi wa ilani, Watendaji kutoka TANROADS pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa daraja hilo.

Mchakato wa ujenzi wa daraja hilo ulianza mwanzoni mwa Agosti 2023 na kufunguliwa Oktoba 15 ,2023 ambapo takribani zaidi ya bilioni 97.1 itatumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo la kisasa pamoja na barabara za maungio zenye Mita 700 pande zote za daraja na kukamilika ndani ya miezi 24

Aidha, Albert Chalamila akizungumza wakati wa hafla hiyo ametoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassani kwa utekelezaji wa mradi huo wenye masilahi mapana kwa umma, pia amempongeza Waziri wa Ujenzi kwa kazi nzuri anayoifanya katika sekta ya ujenzi wa miundombinu katika Mkoa huo na kutoa maombi juu ya ujenzi wa daraja la Mzinga lililopo Wilaya ya Temeke, barabara kibada-mwasonga Kigamboni pamoja na taa za barabarani.

Vilevile Waziri Bashungwa amesema kutakuwa na zaidi ya bilioni 125 zitakazotumika kujenga daraja la Kigogo mita 50, daraja la Mkwajuni mita 20 katika jimbo la Kinondoni, daraja la Nguva eneo la Mikadi- Kigamboni, daraja la Kisarawe na mifereji ya maji Kigamboni Kibada, daraja la JKT Ununio, Mifereji ya maji barabara ya Morroco-Afrikana Mwenge, Mlalakuwa na daraja la Mtongani Jimbo la Kawe daraja la Mbagala rangi tatu kuelekea vikindu na kumwaagiza Mtendaji Mkuu kusimamia ujenzi pamoja na taa za barabarani.

Amesema ujenzi wa madaraja hayo utafungua njia kwa maendeleo makubwa jijini Dar es Salaam na Taifa kwa unumla, kurahisisha usafiri, kuongeza ajira, na kuimarisha uchumi pia kupunguza foleni, kuboresha usalama, na kuharakisha huduma muhimu, hivyo kuchangia maendeleo makubwa na ustawi wa jamii.

Leave a Reply