You are currently viewing Vyama 14 vya siasa vyatangaza kushiriki uchaguzi mkuu

Vyama 14 vya siasa vyatangaza kushiriki uchaguzi mkuu

Vuguvugu la uchaguzi mkuu nchini linaendelea kupamba moto baada vyama 14 vya siasa vya upinzani kuungana na kuunda jukwaa maalumu kwa lengo la kuisisitizia Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC),  kuwataarifu na kutangaza wagombea watakaoshinda katika Uchaguzi Mkuu unaokuja.

Mbali na hayo vyama hivyo vimesema vinaendelea na majadiliano ndani ya vyama vyao kuhusu uwezekano wa kuungana katika uchaguzi huo.

Iwapo vitafikia muafaka itakuwa si mara ya kwanza kwa vyama vya siasa nchini kuunda umoja wakati wa uchaguzi, ambapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015  vyama vinne vya NLD, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF vilishiriki uchaguzi huo kupitia Ukawa. 

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, vyama hivyo vilimsimamisha  Edward Lowassa kuwa mgombea urais huku vikigawana majimbo ya kusimamisha wagombea.

Vyama vilivyoko katika jukwaa hilo jipya ni 14 kati ya 18 vilivyosaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Vyama hivyo ni ADA-TADEA, DP, NRA, NCCR-Mageuzi, UDP, AAFP, UMD, MAKINI, CUF, NLD, CCK, UPDP, TLP na SAU. Baadhi ya vyama hivyo tayari vimeteua wagombea urais.

Leave a Reply