You are currently viewing Wakulima wajipatia  bilioni 347 kutoka NFRA

Wakulima wajipatia  bilioni 347 kutoka NFRA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakulima wa Tanzania wanaozalisha  mazao ya chakula na kuyauza kwa Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula Nchini (NFRA)  wamelipwa bilioni 347   katika miezi minane iliyopita kuanzia  mwezi Julai 2024 hadi mwezi huu.

Akitoa taarifa hapa juu ya ununuzi wa mazao katika msimu uliopita, uimarishaji wa wakala kuelekea kujitegemea na matazamio katika msimu wa ununuzi wa mazao ujao,  Mkurugenzi Mkuu wa NFRA,  Dkt Andrew Komba, alisema malipo yote yamekamilika na kwamba hakuna mkulima ambaye anaendelea kuidai NFRA.

“Endapo kuna mtu atasema kuwa bado anatudai hela basi atakua hajafuatilia taarifa za malipo katika akaunti yake  au kuna baadhi ya taarifa zake hakuzihakiki vyema. Lakini kwa upande wetu tumelipa madeni yote na kwa sasa tunaenda kuanza msimu mpya wa manunuzi tukiwa hatuna deni kutoka kwa wakulima,” alisema Dkt Komba.

Dk. Komba alieleza kuwa  jukumu la NFRA ni kuhakikisha usalama wa chakula nchini kwa kuhakikisha taifa lina shehena ya mazao yakutosha  hata kama nchi inapitia  changamoto za njaa au majanga ya muda mrefu.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Dkt Andrew Komba akisisitiza jambo kwa wanahabari kwamba Wakala umeshawalipa wakulima wote pesa zao kiasi cha shilingi 347 ambazo walikuwa wadai baada ya kuuza mazao Yako Jijini Dar es Salaam.

Alisema katika kutekeleza jukumu hilo, NFRA imekua ikinunua kidijitali mazao ya nayozalishwa na Watanzania na kuyahifadhi katika maghara yake.

“Miongoni mwa mazao ambayo tumekua tukinunua kutoka kwa wakulima ni pamoja na mahindi, mtama, mchele,dengu pamoja na mbaazi,” alifafanua na kuongeza kwamba  NFRA ina madaraka ya kuuza mazao nje. Amesema mpaka sasa NAFRA imeuza takribani tani 600,000  katika masoko ya kimataifa katika nchi za China, India, Congo DRC, Zambia, Malawi, Zimbabwe na Msumbiji.

Amefafanua kuwa kwa  mauzo hayo ya nje NFRA imekusanya takribani bilioni 540 na fedha hiyo imetumika kulipa  mikopo benki, kukarabati maghala na barabara na pia kuwalipa  wakulima kwa mazao.

Amesema  NFRA imevunja rekodi kwa  kukusanya tani za mazao ambazo hazikupata kukusanywa. Amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 NFRA ilikuwa na uwezo wa kuhifadhi takribani tani 351,000.  Lakini  sasa NFRA inahifadhi tani 776,000 katika maghala yake.

“Ili kuhakikisha nchi inakuwa na hifadhi ya kutosha Rais Dkt Samia aliiwekea NFRA lengo la kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030. Hivyo jitihada za kulifikia lengo hilo zimekuwa zikiongozwa na Rais Samia mwenyewe pamoja na Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe.  Na sisi wanafanyakazi wa NFRA tumekuwa tukishirikiana ili tulifikie lengo hilo,”alisema Dkt Komba.

Alifafanua kuwa tani 300,000 zitabakishwa katika maghala kwa ajili ya usalama wa chakula nchini. Kwa maana ya kwamba ikitokea uzalishaji wa chakula ukapungua basi NFRA itakuwa na uwezo wa kulilisha taifa kwa mwaka mzima.

Aidha, ili NFRA iweze kujiendesha yenyewe kama taasisi ilianza kufanya biashara ya kuuza shehena ya mazao katika masoko ya kimataifa yakiwemo China, India, Congo DRC, Zambia, Malawi, Zimbabwe, Msumbiji pamoja na Malawi.

“Njia hii ya kuuza mazao imekua  ni biashara yenye tija kwa Wakala kwani tumeweza kuuza mazao yenye thamani ya bilioni 540 ambapo katika  pesa bilioni 347 zimetumika kuwalipa wakulima  na kufanya ukarabati wa miundombinu ya majengo na barabara,” alisema Dk. Komba

Amesisitiza  kuwa kati ya tani 7760,000 ni tani 400,000 tu zitauzwa katika masoko ya ndani na nje  na tani 300,000 hazitouzwa ili kulinda usalama wa chakula nchini.

Ikumbukwe kuwa kuna wakati  NFRA ililalamikiwa kwa kutowalipa  wakulima kwa wakati, lakini Dkt Komba amesema hadi Desemba mwaka jana NFRA ilikwisha walipa wakulima wote.

Leave a Reply