Tunaposema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Sikivu tunamaanisha.Hii limedhiirika baada ya Serikali kupokea na kuahidi kuyafanyia kazi maombi ya wasafirishaji.
Wasafirishaji hao wakiwemo wamiliki wa mabasi ya masafa marefu na daladala walipanga kufanya mgomo kesho Jumapili (Aprili 12) kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu kutokana na bei za mafuta.
Kwa kutambua hilo, Serikali ya awamu sita kupitia Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amekutana na wadau hao na kuahidi kuzifanyi kazi changamoto zote zinazowakabili.
“Tarehe 8 tuliotoa rai ya kusisitisha usafiri, lakini bahati nzuri Serikali sikivu inayongozwa na Dkt Samia imetuma Waziri Mbarawa kutusikiliza, tulikuwa na kikao kizuri, tumesikilizana matatizo yetu na wameyachukua na kuyafanyia kazi,” amesema Priscu John Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania.
Wamiliki hao wametoa hofu abiria nchini wakiwataka kuendelea na mchakato wa kufanya ‘booking’ za safari kwa kuwa usafiri utakuwepo.
