You are currently viewing Wenje: Vijana mna wajibu kuilinda Tanzania
Screenshot

Wenje: Vijana mna wajibu kuilinda Tanzania

Mwanasiasa na mbunge wa zamani wa Nyamagana mkoani Mwanza,  Ezekia Wenje amesema vijana wana wajibu wa kulinda nchi bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

Amesema hayo leo , Jumamosi Mei 16,2926  katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu ‘never again’ tuipende, tuitunze , tuilinde  nchi yetu’ lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na TAHLISO mkoani hapa.

Wenje amesema kwa takwimu zilizopo vijana nd ndio wengi na  mchango mkubwa katika Taifa na ndio watu wanaouweza kuamua hatima ya nchi.

” Kuna tofauti kati ya Serikali na Taifa Kuna tofauti kati ya nchi na Serikali, duniani hapa Serikali zinapita, chukua mfano Marekani kuna wakati Democratic kinaongoza, wakati mwingine Republican, lakini msingi lazima Taifa libaki,” amesema Wenje na kuongeza kuwa;

” Tunaposema never again, tunafanya marejesho kilichotokea Oktoba 29,2025, ndio maama nasema kuna utofauti kati ya nchi na Serikali.Ukiwa kijana lazima ujue bila kuzingatia chama unachotoka, jukumu lako namba moja ni kulinda nchi,” amesema

Wenje amesema ikitokea umeichoma nchi hata  Serikali ikiondoka utabaki na nini? Hivyo vijana wa Kitanzania wana jukumu la kuilinda Tanzania bila kujali wametokea wapi kwa sababu Tanzania ni moja.