You are currently viewing Zaipuna kwenye hafla ya kumkabidhi Rais Samia Tuzo

Zaipuna kwenye hafla ya kumkabidhi Rais Samia Tuzo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna ameshiriki hafla ya kumkabidhi tuzo maalum Rais Samia Suluhu Hassan iliyoandaliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bunge la Tanzania limemtunuku Rais Samia tuzo maalumu ya heshima ya kutambua mchango wake kwa maendeleo ya Taifa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwake leo Jumamosi Mei 31 na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa niaba ya wabunge, kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Rais Samia aliapishwa kushika wadhifa huo, Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa tano, Hayati Dk John Magufuli, kilichotokea Machi 18, 2025.

Leave a Reply