Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Magu, Joshua Nassari ameibuka mshindi katika kura za maoni za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CCM kwa kupata kura 6,678.
Katika matokeo hayo wagombea waliofuata na kura zao kwenye mabano ni pamoja na Dk. John D. Pallangyo (652), Elisa Mbisse (650), Prof. Daniel Pallangyo (372), Johnson Sarakikya (312), William Sarakikya (307), Anjela Pallangyo (105) na Rose Urioh (55)
BITEKO APATA 99.8% BUKOMBE
Wajumbe wa Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe wamemchagua Dkt. Doto Mashaka Biteko kwa asilimia 99.8 baada ya kupata kura 7,441 kati ya kura 7,456 zilizopigwa ili apeperushe bendera ya Chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo jana August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Bukombe linajumla ya wajumbe 7,835 na waliopiga kura ni 7,456 ambapo kura zilizoharibika ni 15, kura za hapana ni 0, kura halali zilizopigwa ni 7,441.
Kwa matokeo hayo, Dkt. Doto Mashaka Biteko amepata kura 7,441 kati ya 7,456 sawa na wastani wa asilimia 99.8 uchaguzi uliofanyika katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
