Ujumbe wa Kamati Ndogo ya Afrika ya Bunge la Wawakilishi la Marekani, umesema utakuja kuitembelea Tanzania mwaka 2026 ili kuimarisha ushirikiano zaidi ya baina ya mataifa hayo mawili.
Mwanachama wa Kamati Ndogo ya Afrika ya Bunge la Wawakilishi la Marekani, Dkt. Ronny Jackson amemueleza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo kuwa wanavutiwa na nchi ya Tanzania hivyo wanafikiria kuja na ujumbe wake.

Kwa mujibu wa Dkt Jackson amewahi kufika Tanzania na anavutiwa na uzuri wa nchi, na pia anafikiria kuongoza ujumbe utakaojumuisha wabunge wengine kuja nchi Tanzania mwaka 2026 baada ya kupata mwaliko wa Balozi Kombo.
Dkt Jackson ameeleza leo Desemba 16,2025 hayo wakati wa kikao chake na Balozi Kombo ambaye yupo ziarani Marekani katika mwendelezo wa kufanya mikutano na viongozi na wadau mbalimbali muhimu ili kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Taifa hilo.
