You are currently viewing ‘Camp’ ya macho CCBRT Mbagala yavuta mamia ya wakazi wenye matatizo

‘Camp’ ya macho CCBRT Mbagala yavuta mamia ya wakazi wenye matatizo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAELFU ya wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake katika Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kupima macho, kupata ushauri nasaha sambamba na kupata matibabu stahiki yalitolewa bure Hospitali ya CCBRT jana Jumamosi.

 Huduma hiyo ya macho na ushauri nasaha ni mpango endelevu wa Hospitali ya CCBRT kupambana na kutokomeza matatizo macho miongoni mwa Watanzania na kuzuia upofu usio wa lazima.

Mratibu wa mafunzo ya Mama na Mtoto kutoka CCBRT, Dkt. Timothy Mushi (kulia) akitoa elimu ya afya ya macho na umuhimu wa uchunguzi wa mara kwa mara kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye kambi ya siku mbili ya upimaji macho inayotolewa bure kwenye Viwanja vya Mbagara Zakhem, jijini Dar es Salaam.

“Tumefurahishwa sana kwani watu wengi wamejitokeza kuja kupima macho, kupata ushauri nasaha na matibu bure,”Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii na Utafiti, Bi. Rhoda Ndakwe amesema na kuongeza kuwa uhitaji wa huduma hiyo ni mkubwa kutokana na idadi ya watu waliojitokeza.

Bi. Rhoda ambaye alimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Brenda Msangi amesema CCBRT imejiwekea utaratibu wake kutoa huduma ya macho na ushauri ili kusaidia jamii kuepukana na ulemavu wa macho ikiwemo upofu.

Bi. Rhoda hakusita kuwataja  Shirika la Christian Blind Mission (CBM) likishirikiana CCBRT kufanikisha zoezi hilo na kutoa wito Kwa wadau wengi zaidi wajitokeze kudhamini zoezi kama hilo ili kuwafikia wahitaji wengi hapa nchini na kuwashukuru wafadhili mbalimbali wakiwemo CBM, Light For The World (LFTW).

“CCBRT kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunalenga kutoa huduma  muhimu za macho ikiwemo kuwatambua mapema wenye ‘ Clacoma’,’Cataract’ na ndiyo maana tukaweka kambi kama hizi.

“Tunapenda kuwagundua mapema na kuhakikisha wanapata matibu mapema Alisema na kuongeza kuwa CCBRT ipo imara kuhakikisha inazuia ulemavu wa macho kwa Watanzania.

Hospitali ya CCBRT ni miongoni mwa hospitali chache hapa nchini zinazotoa huduma mbalimbali  za kibobezi zikiwemo   Huduma za macho, festula,huduma za  figo na usafishaji Figo, huduma za mifupa, Huduma za uzazi na magonjwa ya wanawake, huduma za  upasuaji pamoja  radiolojia  na nyingine nyingi.