You are currently viewing ATCL yapata hasara ya Sh bilioni 748 tangu ianzishwe
Air Tanzania

ATCL yapata hasara ya Sh bilioni 748 tangu ianzishwe

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara katika ukaguzi wa mwaka wa fedha wa 2024/25.

Kichere ameyasema hayo hii leo tarehe 30 Machi 2026, alipokuwa akiwasilisha ripoti yake ya ukaguzi wa fedha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa pamoja na kupokea ruzuku ya mishara na gharama za uendeshaji kutoka Serikalini, kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, Shirika hilo limetengeneza hasara ya shilingi 191,19 Bilioni.

“Kampuni ya Ndege ya ATCL imeendelea kupata hasara, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ilipata hasara ya shilingi 191.19 bilioni, ikiwa ni ongezeko la silimia 108,” alisema Kichere

Aidha alisema kuwa ongezeko hilo limesababisha Shirika hilo kufikisha jumla ya hasara ya shilingi 748 Bilioni toka lilipoanzishwa.

“Ongezeko hilo limefanya kufikisha jumla ya hasara taingia lianzishwe ya shilingi bilioni 748, licha ya kupokea ruzuku ya Serikali kwa ajili ya mishahara na gharama za uendeshaji,” alisema mkaguzi huyo.