Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto, amesema Kampuni 500 za Kenya zimewekeza Dola za Marekani bilioni 1.7 nchini Tanzania.
Amesema uwekezaji huo umeongeza ajira za mamilioni ya watu na kukuza mapato makubwa kwa serikali.
Rais Ruto ameyasema hayo leo Aprili 5, 2026, wakati akihutubia Bunge la Tanzania jijini Dodoma na kuongeza kuwa uwekezaji unaonesha kuimarika kwa uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo jirani.
Kadhalika, amesema masharikiano hayo pia yapo kwa kampuni za Kitanzania ambazo zimepanua shughuli za uwekezaji nchini Kenya.
Amezitaja Taifa Gas, Amson Group na Lake Gas kama mifano ya kampuni zilizowekeza nchini Kenya.
Amesema uwekezaji huo wa miaka mitatu lakini wanaamini unaendelea kukuza na kuongeza uchumi wa mataifa hayo mawili kwa kasi kubwa.
“Kampuni kutoka Tanzania pia zimewekeza Kenya na niliwaambia Wakenya kwamba mwekezaji kutoka Tanzania ni mshirika wetu, wanatuletea pesa na tunatafuta muda mrefu kutafuta wawekezaji,” amesema Ruto na kuongeza zaidi kuwa;
“Nilimpa mpatia Mtanzania kiwanda cha uwekezaji kuna watu walilalama, wale walioniuliza kwanini Watanzania wamewekeza Kenya, niliwauliza awali kampuni ilimilikiwa na Wafaransa sasa inamalikiwa na Mtanzania kwanini hamkulalama kumilikiwa na Wafaransa,” amesema Ruto.
